Al-Muzzammil 73:18
المزملٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرٌۢ بِهِۦ ۚ كَانَ وَعْدُهُۥ مَفْعُولًا
Hapo mbingu zitapasuka kwa sababu yake! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa. [18]
[18] Mbingu juu ya nguvu zake na ukubwa wake, Siku hiyo zitapasukilia mbali kwa shida zake na vitisho vyake. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itokee, hapana hivi wala hivi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mbingu zitapasuka Siku hiyo, kwa ukubwa wa janga lake, hakika ahadi ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ya kuwa Siku hiyo itakuja ni yenye kutimia bila shaka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net