Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 73 · Aya ya 11

Al-Muzzammil 73:11

المزمل

وَذَرْنِى وَٱلْمُكَذِّبِينَ أُو۟لِى ٱلنَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا

Maana

Na niache Mimi na hao wanaokanusha, walioneemeka; na wape muhula kidogo!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo! [11]

[11] Niachilie Mimi hao wanao kadhibisha, wenye kuneemeshwa, na uwape muhula muda mfupi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uniache mimi, (ewe Mtume), na hawa wakanushaji wa aya zangu, wenye starehe na kubobea kwenye ulimwengu, na uwape mhula wa muda mchache kwa kucheleweshewa adhabu mpaka muda wa wao kuadhibiwa ufike.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muzzammil

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net