Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 73 · Aya ya 10

Al-Muzzammil 73:10

المزمل

وَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا

Maana

Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri. [10]

[10] Na vumilia upuuzi wanao usema, na jitenge nao kwa moyo wako, na nenda kinyume na vitendo vyao, pamoja na kuwapuuza, na kuacha kujilipizia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uvumilie kwa yale ambayo washirikina wanayasema kuhusu wewe na kuhusu Dini yako. Na uende kinyume na wao katika maneno yao ya ubatilifu pamoja na kuwapuuza na kuacha kuwarudishia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muzzammil

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net