Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 99

Al-A'raaf 7:99

الأعراف

أَفَأَمِنُوا۟ مَكْرَ ٱللَّهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْقَوْمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

. Je, wamejiaminisha na mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye kukhasiri. [99]

[99] Je, hawaujui mwendo wa Mwenyezi Mungu anavyo kwenda nao wanao kanusha, hata wakajitumainisha kuwa haitowafikia adhabu usiku au mchana? Naye, huipeleka kwa mpango wake wasio uona watu. Hakika hawawi wajinga wa mpango na mwendo wa Mwenyezi Mungu katika kuadhibu ila wale wanao kanusha, wenye kuzikhasiri nafsi zao kwa kutozinduka katika mambo yaliyo khusu kufanikiwa kwao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wamejiaminisha, watu wa miji iliyokanusha, na vitimbi vya Allah Mtukufu kwao na kuwapa Kwake wao muhula, kwa kuwaachilia na yale Aliyowaneemesha nayo katika dunia yao, kwa njia ya kuwatesa sababu ya vitimbi vyao? Basi hawajiaminishi na vitimbi vya Allah Mtukufu isipokuwa watu wenye kuangamia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net