Al-A'raaf 7:98
الأعرافأَوَأَمِنَ أَهْلُ ٱلْقُرَىٰٓ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ
Au wakazi wa mijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu mchana hali ya kuwa wanacheza?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika mchana, nao wanacheza? [98]
[98] Je, watu hawa wameghafilika na wamejiaminisha kuwa adhabu haitawajia mchana kweupe na jua linawaka, nao wameshughulikia mambo yasiyo na faida nao?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au kwani wanajiaminisha watu wa mijini kuwa wamesalimika na adhabu ya Allah Mtukufu kuwa haitawafika kipindi cha mchana wakiwa wameghafilika, wameshughulika na mambo ya dunia yao? Allah Mtukufu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuzitaja, kwa kuwa wanadamu nyakati hizi huwa wameghafilika zaidi, kwa hivyo kuja adhabu katika nyakati hizi huwa na kitisho zaidi na ni kali zaidi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net