Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 97

Al-A'raaf 7:97

الأعراف

أَفَأَمِنَ أَهْلُ ٱلْقُرَىٰٓ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَـٰتًا وَهُمْ نَآئِمُونَ

Maana

Je, wakazi wa mijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu usiku hali ya kuwa wamelala?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika usiku, nao wamelala? [97]

[97] Je, watu wa hii miji walio letewa wito wa Manabii wao na wasiwaamini, wamejiaminisha kuwa adhabu yetu haitawafika nao wamezama katika usingizi wao?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani wanadhani hawa watu wa mijini kuwa wao wameokoka na wamesalimika na adhabu ya Allah Mtukufu kuwa haitawafika kipindi cha usiku wakiwa wamelala?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net