Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 96

Al-A'raaf 7:96

الأعراف

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ ٱلْقُرَىٰٓ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّقَوْا۟ لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَـٰتٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا۟ فَأَخَذْنَـٰهُم بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Maana

Na lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, basi hakika tungeliwafungulia baraka za kutoka mbinguni na ardhini. Lakini walikadhibisha, basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma. [96]

[96] Na lau kuwa watu wa hiyo miji wangeliamini walio kuja nayo Mitume, na wakatenda walio wausia, na wakajitenga na aliyo yaharimisha Mwenyezi Mungu, tungeli wapa baraka nyingi zitokazo mbinguni na kwenye ardhi, kama mvua, na mimea, na matunda, na wanyama, na riziki, na amani na kusalimika na misiba. Lakini wao wakapinga na wakawakadhibisha Mitume. Basi tukawapatiliza kwa adhabu nao wamelala, kwa sababu ya ukafiri na maasi waliyo yazua. Basi huko kushikwa waliko shikwa kwa adhabu ni matokeo ya lazima kuwa kwa ajili ya maovu waliyo yachuma, na yawe kuwa ni somo kwa walio kama wao ikiwa wanayatia akilini!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau watu wa miji wangewaamini Mitume wao wakawafuata na kujiepusha na aliyoyakataza Allah Mtukufu, Angaliwafungulia Allah Mtukufu milango ya heri kwa kila njia. Lakini wao walikanusha, Allah Mtukufu Akawatesa kwa adhabu yenye kuangamiza kwa sababu ya ukafiri wao na maasia yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net