Al-A'raaf 7:100
الأعرافأَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلْأَرْضَ مِنۢ بَعْدِ أَهْلِهَآ أَن لَّوْ نَشَآءُ أَصَبْنَـٰهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ
Kwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya waliokuwa wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao, na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawahidiki hawa wanao rithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tutawapatiliza kwa madhambi yao, na tutapiga muhuri juu ya nyoyo zao, na kwa hivyo hawatasikia?. [100]
[100] Je, hawaujui mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa kaumu zilizo kwisha pita kabla yao, na kuwa shani yetu kwao ni kama ilivyo kuwa kwa walio watangulia? Na kwamba wao lazima wafuate tuyatakayo. Tukitaka kuwaadhibu kwa sababu ya madhambi yao tutawapatiliza kama tulivyo wapatiliza walio kama wao. Nasi tunatia muhuri nyoyo zao kwa kuwa zimeharibika bila ya kiasi, mpaka ikafika ukomo kuwa hazipokei tena uwongofu. Kwa muhuri huo imekuwa hawasikii hikima wala nasiha, kwa msikio wa kufahamu na kuwaidhika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani haikuwafunukia wale waliokaa kwenye nchi baada ya watu wake waliopita kuangamizwa kwa maasia yao, na wakafuata miendo yao, kwamba lau tungetaka tungaliwaadhibu kwa makosa yao, kama tulivyowafanyia waliopita kabla yao, na kwamba tutazipiga chapa nyoyo zao, haki isiingie na wasisikie mawaidha wala makumbusho?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net