Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 101

Al-A'raaf 7:101

الأعراف

تِلْكَ ٱلْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنۢبَآئِهَا ۚ وَلَقَدْ جَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَمَا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوا۟ بِمَا كَذَّبُوا۟ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Miji hiyo, tunakusimulia katika habari zake. Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba nyoyo za makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Miji hiyo, tunakusimulia baadhi ya khabari zake. Na hapana shaka Mitume wao waliwafikia kwa hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini waliyo yakanusha zamani. Namna hivi Mwenyezi Mungu anazipiga muhuri nyoyo za makafiri. [101]

[101] Hiyo ni miji iliyo dumu karne nyingi, na imepitiwa na muda mrefu katika taarikhi yao. Tunakusimulia hivi sasa baadhi ya khabari zao zenye somo la kuzingatiwa. Na watu wa miji hiyo walifikiwa na Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi zenye kuonyesha ukweli wa wito wao. Lakini haikuwa shani yao kuamini baada ya kuja hizo Ishara zilizo wazi, kwa sababu ya mtindo wao wa kuwakanusha wasemao kweli. Basi wakawakadhibisha Mitume wao, wala hawakuongoka! Basi ni hivyo Mwenyezi Mungu huweka kizuizi juu ya nyoyo na akili za makafiri, ikafichika kwao Njia ya Haki, na wakajitenga nayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Miji hiyo iliyotangulia kutajwa, nayo ni miji ya watu wa Nûh, Hûd, Sãlih, lût, na Shu‛ayb, tunakupatia, ewe Mtume, habari zake na zile zinazohusu mambo ya Mitume wa Allah Mtukufu waliotumwa kwa watu wa miji hiyo, zinazofanya mazingatio yapatikane kwa wenye kuzingatia na pia makemeo kwa madhalimu. Hakika watu wa miji hiyo walijiwa na Mitume wetu na hoja zilizo wazi juu ya ukweli wao, lakini hawakuwa ni wenye kuyaamini yale waliyokuja nayo hao Mitume kwao kwa sababu ya kupita mipaka kwao na kuikanusha haki. Na mfano Alivyopiga chapa Allah Mtukufu kwenye nyoyo za makafiri hawa waliotajwa, Atapiga mhuri kwenye nyoyo za wenye kumkanusha Muhammad (sala na salamu zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net