Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 102

Al-A'raaf 7:102

الأعراف

وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَآ أَكْثَرَهُمْ لَفَـٰسِقِينَ

Maana

Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye kushika agano lolote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hatukuwaona wengi wao kuwa wanatimiza ahadi; bali kwa hakika tuliwakuta wengi wao ni wapotofu. [102]

[102] Wala hatukuwakuta wengi wa watu hao kuwa ni wenye kutimiza ahadi kwa Imani tulio wausia kwa ndimi za Mitume, na yanayo tambuliwa na akili na nadhari nzuri. Na mwendo ulio thibiti kwao ni vile kuselelea katika upotofu na kwenda kinyume na kila ahadi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hatukuwapata wengi wa watu waliopita kuwa wana uaminifu wala utekelezaji ahadi, na hatukuwapata wengi wao isipokuwa ni watokaji nje ya utiifu wa Allah Mtukufu na ufuataji amri Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net