Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 103

Al-A'raaf 7:103

الأعراف

ثُمَّ بَعَثْنَا مِنۢ بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَظَلَمُوا۟ بِهَا ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Kisha tukamtuma baada yao Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazifanyia dhuluma. Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha baada yao tukamtuma Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazikataa. Basi tazama ulikuwaje mwisho wa waharibifu. [103]

[103] Tena baada ya Mitume hao tulimtuma Musa a.s. Naye akaja na dalili zenye kuonyesha ukweli wa anayo yafikisha kutokana nasi kumpelekea Firauni na kaumu yake. Musa akaufikisha wito wa Mola wake Mlezi, na akawaonyesha Ishara ya Mwenyezi Mungu. Nao wakadhulumu nafsi zao na watu wao kwa kuzikataa kwa kiburi na upinzani tu! Basi wakastahiki adhabu kali kutokana na Mwenyezi Mungu, na hivyo ukawa mwisho wa mambo yao! Basi ewe Nabii! Angalia vyema mwisho wa mafisadi katika ardhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tulimtuma, baada ya Mitume waliotangulia kutajwa, Mûsã mwana wa ‛Imrãn kwa miujiza yetu iliyo wazi aende kwa Fir‛awn na watu wake, wakaikataa na kuikanusha kwa udhalimu na upinzani. Tazama kwa mazingatio, namna gani tuliwafanya na tuliwazamisha hadi wa mwisho wao, huku Mûsã na watu wake wakiona? Na huo ndio mwisho wa waharibifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net