Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 91

Al-A'raaf 7:91

الأعراف

فَأَخَذَتْهُمُ ٱلرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا۟ فِى دَارِهِمْ جَـٰثِمِينَ

Maana

Basi tetemeko la ardhi likawachukua, kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na wakaamkia majumbani mwao wamejifudikiza, wamekwisha kufa. [91]

[91] Basi hapo kauli ya kuteremka adhabu ikawa imethibiti. Wakasibiwa kwa tetemeko lilio tikisa nyoyo zao, wakawa katika majumba yao wamesinukia kifudifudi hawana tena uhai.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo watu wa Shu‛ayb wakashikwa na mtetemeko mkali, wakawa wameangushwa kwenye mji wao hali ya kuwa wamekufa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net