Al-A'raaf 7:90
الأعرافوَقَالَ ٱلْمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ لَئِنِ ٱتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَـٰسِرُونَ
Na wakasema waheshimiwa waliokufuru katika kaumu yake, "Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waheshimiwa walio kufuru katika kaumu yake wakasema: Mkimfuata Shua'ib, basi hakika hapo nyinyi mtakuwa mlio khasiri. [90]
[90] Hapo basi wale watu walikata tamaa ya kuwafanya Shua'ib na walio kuwa naye wawafuate wao. Na wakajua kuwa hakika hao walikuwa wamethibiti katika Dini yao. Kadhaalika waliogopa wasizidi kuwa wengi wale walio hidika pamoja na Shua'ib kwa kudhihiri nguvu zake na kuthibiti kwake juu ya wito wake. Kwa hivyo wale waheshimiwa wa kikafiri wakawaelekea wafwasi wao wakiwatisha kwa kusema: Wallahi! Mkimfuata Shua'ib mkakubali wito wake, basi hapana shaka nyinyi utakutokeni utukufu wenu na utajiri wenu kwa kufuata dini potovu wasio kuwa wakiifuata wazee wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema wakubwa wenye kukanusha, wenye kupinga ulinganizi wa Tawḥîd (kumpwekesha Allah Mtukufu) waliofikia kiwango cha juu katika ujeuri na uasi, wakitahadharisha kwamba Shu‛ayb asifuatwe, «Kwa hakika, lau mnamfuata Shu‛ayb, nyinyi kwa hivyo ni wenye kuangamia».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net