Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 92

Al-A'raaf 7:92

الأعراف

ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا۟ فِيهَا ۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ شُعَيْبًا كَانُوا۟ هُمُ ٱلْخَـٰسِرِينَ

Maana

Wale waliomkadhibisha Shu'aib ni kama kwamba hawakuishi humo. Wale waliomkadhibisha Shu'aib walikuwa ndio waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale walio mkanusha Shua'ib wakawa kama kwamba hawakuwako. Walio mkanusha Shua'ib ndio walio kuwa wenye kukhasiri. [92]

[92] Hii ndio shani ya Mwenyezi Mungu na hao walio mkanusha Shua'ib, na wakamtishia, na wakamwonya kuwa watamfukuza katika mji wao, na wakafanya kila kitu kuupinga wito wake. Wamehiliki wao na ukahiliki mji wao, ikawa kama kwamba humo hawakuwahi kuishi wale walio mkadhibisha Shua'ib na wakadai kuwa ati atakaye mfuata atakuwa amekhasiri, na wakatilia nguvu madai hayo. Na lililo kuwa ni kuwa wao ndio walio poteza neema yao ya dunia na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao walimkanusha Shu‛ayb walikuwa kama kwamba hawakukaa kwenye nyumba zao wala hawakustarehe humo. Kwani walimalizwa, haikubaki alama yoyote yao, wakapatikana na hasara na maangamivu duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net