Al-A'raaf 7:61
الأعرافقَالَ يَـٰقَوْمِ لَيْسَ بِى ضَلَـٰلَةٌ وَلَـٰكِنِّى رَسُولٌ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Akasema: Enyi watu wangu! Mimi siko katika upotovu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. [61]
[61] Nuhu akawaambia kukataa yale waliyo msingizia: Mimi sina upotofu kama mnavyo dai. Lakini mimi ni Mtume niliye toka kwa Muumba wa viumbe vyote, basi hayumkini awe mbali na haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nûḥ Akasema, «Enyi watu wangu, mimi si mpotevu katika jambo lolote kwa njia yoyote, lakini mimi ni mjumbe kutoka Mola wa viumbe wote; Mola wangu na Mola wenu na Mola wa viumbe wote».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net