Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 60

Al-A'raaf 7:60

الأعراف

قَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotovu ulio dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhaahiri. [60]

[60] Wakasema wale wahishimiwa wao, watu wa mbele mbele na uwongozi katika wao, wakiujibu ule wito wake wa Tawhidi na Siku ya Akhera: Hakika sisi tunakuona wewe uko mbali kabisa na hiyo haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mabwana wao na wakubwa wao walisema, «Sisi tunaitakidi, ewe Nûḥ, wewe uko kwenye upotevu waziwazi uko kando ya njia sawa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net