Al-A'raaf 7:59
الأعرافلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦ فَقَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥٓ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Hakika, tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku iliyo kuu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu. [59]
[59] Washirikina wakafanya inda, na wakaikanusha Haki ilipo wajia kwa hoja za kukata zisio pingika. Lakini huo ndio mtindo wa makafiri kwa Manabii wao tangu zamani. Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake alio tokana nao. Naye akawakumbusha kuwa yeye ni mmoja wao: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake. Kwani nyinyi hamna Mungu asiye kuwa huyu. Na mjue kuwa kutakuwapo kufufuliwa na kuhisabiwa Siku ya Kiyama. Na hiyo ni Siku adhimu. Mimi nakukhofieni Siku hiyo msije mkapata adhabu kali kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tulimtuma Nûḥ kwa watu wake, ili awalinganie kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, na kumtakasia ibada, akasema, «Enyi watu wangu, muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake, na mumnyenyekee kwa kumtii, nyinyi hamna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada.Msipofanya na mkasalia kwenye kuabudu masanamu yenu, hakika mimi nawaogopea msishukiwe na adhabu ya Siku ambayo shida yenu itakuwa kubwa, nayo ni Siku ya Kiyama».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net