Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 58

Al-A'raaf 7:58

الأعراف

وَٱلْبَلَدُ ٱلطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُۥ بِإِذْنِ رَبِّهِۦ ۖ وَٱلَّذِى خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ

Maana

Na ardhi nzuri mimea hutoka yake kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Nayo ardhi ambayo ni mbaya haitoki isipokuwa mimea michache, isiyokuwa na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ardhi njema, yenye udongo wa rutba, hutoa mimea yenye kukua vizuri yenye uhai, kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Na ardhi mbaya haitoi ila mimea michache, isiyo na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyo zipambanua Ishara (Aya) kwa watu wanao shukuru. [58]

[58] Na ardhi njema yenye rutba nzuri huzalisha mimea inayo kua kwa nguvu, kwa idhini ya Mola Mlezi. Na ardhi mbaya haitoi ila mimea michache, isiyo na faida, ambayo huwa ndio sababu ya dhiki ya huyo mkulima.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ardhi nzuri, ikiteremkiwa na mvua, inatoa mimea kwa idhini ya Allah Mtukufu na matakwa Yake, ikiwa mizuri na kwa njia ya wepesi. Hivyo ndivyo alivyo Muumini, zikiteremka aya za Allah Mtukufu kwake, hunufaika nazo na huzalisha kwake maisha mema. Ama ardhi ya chumvi iliyo mbovu; hiyo haitoi mimea isipokuwa mibovu isiyokuwa na faida, tena kwa shida, na haitoi mimea mizuri. Hivyo ndivyo alivyo kafiri, hanufaiki kwa aya za Allah Mtukufu. Mfano wa sampuli hiyo nzuri katika kueleza, ndiyo namna tunavyoleta hoja na dalili mbalimbali kuthibitisha haki kwa watu wanaozishukuru neema za Allah Mtukufu na wanaomtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net