Al-A'raaf 7:57
الأعرافوَهُوَ ٱلَّذِى يُرْسِلُ ٱلرِّيَـٰحَ بُشْرًۢا بَيْنَ يَدَىْ رَحْمَتِهِۦ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَـٰهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ ٱلْمَآءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِۦ مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ ٱلْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Na Yeye ndiye anayetuma pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapobeba mawingu mazito, tunayapeleka kwenye nchi iliyokufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, na tukatoa kwayo kila aina ya matunda. Basi namna hiyo ndivyo tunavyowafufua wafu, ili mkumbuke.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndio kama hivyo tukatolesha kila aina ya matunda. Basi hali kadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka. [57]
[57] Na Mwenyezi Mungu, Aliye takasika, Aliye tukuka, peke yake, ndiye anaye zipeleka pepo kubashiria rehema yake, kwa mvua ambazo kwa sababu yake ndio makulima humea, na konde humwagiwa maji. Hizo pepo hubeba mawingu ambayo nayo yamebeba maji. Tunayachunga mpaka yafike kwenye nchi isiyo kuwa na mimea, ambayo ni kama maiti asiye na uhai, yakamiminika maji, na tena Mwenyezi Mungu husabibisha kumea namna kwa namna ya mazao na matunda. Na mfano kama huu wa kuihuisha ardhi kwa mimea, ndivyo tunawafanya maiti wakawa wahai. Haya ni kwa ajili mpate kuikumbuka kudra ya Mwenyezi Mungu, na mpate kuamini kuwa kupo kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Anayetuma upepo mzuri mororo wenye kubashiria mvua ambayo upepo huo unaisukuma kwa idhini ya Allah Mtukufu, na hapo viumbe vikangiwa na furaha kwa hiyo rehema za Allah Mtukufu. Na pindi ifikapo wakati ambapo upepo umebeba mawingu yaliyobebeshwa mvua, Allah Mtukufu Huyapeleka kwa upepo huo ili kuihuisha nchi iliyopigwa na ukame ardhi yake na kukauka miti yake na mimea yake ya nafaka, Allah Mtukufu hapo Akaiteremsha, kwa mawingu hayo, mvua, Akaitoa kwayo nyasi, miti na mimea ya nafaka, na miti ikarudi kujaa sampuli ya matunda. Kama tunavyoihuisha ardhi hii kwa mvua, vilevile tutawatoa wafu kutoka makaburini mwao baada ya kutoweka kwao, ili muwaidhike na mchukulie dalili juu ya upweke wa Allah Mtukufu na uwezo Wake wa kufufua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net