Al-A'raaf 7:56
الأعرافوَلَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَـٰحِهَا وَٱدْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٌ مِّنَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Wala msifanye uharibifu katika dunia baada ya kutengenea kwake. Na mwombeni kwa hofu na kutumai. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wafanyao uzuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema. [56]
[56] Wala msifanye fisadi katika nchi njema kwa kueneza maasi na dhulma na uvamizi. Na muombeni Yeye Subhanahu, Aliye takasika, kwa kuiogopa adhabu yake, na kwa kutumai thawabu zake. Na hakika rehema yake ipo karibu kwa kila mwenye kufanya mema. Na hayo ni hakika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msilete katika ardhi aina yoyote ya uharibifu, baada ya Allah Mtukufu kuitengeneza kwa kutuma Mitume, (amani iwashukie) na kuimarika kwa utiifu wa Allah Mtukufu. Na muombeni Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mkimtakasia maombi yenu, kwa kuogopa mateso Yake na kuwa na matumaini kupata malipo Yake mazuri. Hakika rehema za Allah Mtukufu iko karibu na wenye kufanya wema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net