Al-A'raaf 7:55
الأعرافٱدْعُوا۟ رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْمُعْتَدِينَ
Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka. [55]
[55] Ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, ndiye aliye umba kila kitu peke yake, basi muombeni Yeye tu kwa kumuabudu na kwa mengineyo, mkimtangazia hayo maombi, kwa udhalilifu na kunyenyekea, kwa dhaahiri au bila ya kudhihirisha. Wala msipite mipaka kwa kumshirikisha na wenginewe, au kwa kumdhulumu yeyote. Kwani hakika Mwenyezi Mungu, hawapendi wanao ruka mipaka, na wafanyao uadui.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Muombeni, enyi Waumini, Mola wenu, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa siri na kwa dhahiri.Na maombi yawe kwa unyenyekevu na yawe mbali na kujionyesha.Hakika Allah Mtukufu Hawapendi wanaokiuka mipaka ya sheria Zake. Na ukiukaji mkubwa ni kumshirikisha Allah Mtukufu, kama vile kuwaomba wafu, masanamu na wengineo mfano wao wasiokuwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net