Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 52

Al-A'raaf 7:52

الأعراف

وَلَقَدْ جِئْنَـٰهُم بِكِتَـٰبٍ فَصَّلْنَـٰهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Maana

Na hakika tumewaletea Kitabu tulichokipambanua kwa elimu, uongofu na rehema kwa watu wenye kuamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tumewaletea Kitabu tulicho kipambanua kwa ilimu, uwongofu na rehema kwa watu wenye kuamini. [52]

[52] Na hakika kwa ajili ya kubainisha Haki tuliwapa Kitabu, na tukakipambanua. Kitabu hicho kimekusanya ilimu nyingi, na ndani yake zimo hoja za Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, na Ishara za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu; na pia zimo sharia zake, maelezo ya Njia Iliyo Nyooka, na uwongofu wa kuifikilia. Na pia yamo ndani ya Kitabu hichi mambo ambayo, lau watu wakiyafuata watapata rehema. Na wala hawanufaiki kwacho ila wale ambao ni shani yao kuinyenyekea Haki na kuiamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tumewaletea makafiri Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, tuliyoibainisha, inayokusanya elimu kubwa, yenye kuongoza, kutoa kwenye upotevu, kupeleka kwenye njia ya usawa, hali ya kuwa ni rehema kwa watu wanaomuamini Allah Mtukufu na kuzitumia sheria Zake. Amewahusu wenye kuamini kwa kuwataja, bila ya wengine, Kwa kuwa wao ndio wenye kunufaika nayo

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net