Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 53

Al-A'raaf 7:53

الأعراف

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُۥ ۚ يَوْمَ يَأْتِى تَأْوِيلُهُۥ يَقُولُ ٱلَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَآءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَآءَ فَيَشْفَعُوا۟ لَنَآ أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ ٱلَّذِى كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ

Maana

Je, lipo wanalolingojea isipokuwa matokeo yake? Siku yatatapofika matokeo yake watasema wale waliokisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejihasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, lipo wanalo lingojea isipo kuwa matokeo yake? Siku yatapo fika matokeo yake watasema wale walio kisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyo kuwa yale tuliyo kuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejikhasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua. [53]

[53] Hakika wao hawaiamini hii Qur'ani, na wala hawangojei ila matokeo ambayo Mwenyezi Mungu ameyabainisha kuwa yatawapata wanayo ikataa! Na Siku yatapofika hayo matokeo, nayo ni Siku ya Kiyama, walio ziacha amri zake na maelezo yake, na wakaghafilika kuwa ni waajibu kuiamini, na hali wakiungama madhambi yao, watasema: Hakika walikuja Mitume kutoka kwa Muumba wetu na Mlezi wetu, wakituitia Haki waliyo tumwa kuileta, nasi tukaikataa! Nao wataulizwa: Je, mnao waombezi wakakuombeeni? Nao hawatowapata! Au, je, watarudishwa tena duniani watende mema? Hawatajibiwa! Wamepoteza vitendo vyao kwa kukhadaika na dunia, na umewapotea ule uzushi wa uwongo wa kudai kuna mungu asiye kuwa Allah, Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hakuna wanachokingojea makafiri isipokuwa mateso, ambayo ndiyo kikomo cha mambo yao, waliyoahidiwa katika Qur’ani? Siku kitakapokuja kikomo cha mambo yao, cha kuhesabiwa, kulipwa na mateso Siku ya Kiyama, watasema makafiri walioiacha Qur’ani na wakaikanusha duniani, Sasa imetubainikia kwamba Mitume wa Mola wetu wamekuja na haki na wametupa ushauri mzuri. Je, tunaweza kupata marafiki na waombezi wapate kutuombea kwa Mola wetu? Au tunaweza kupewa nafasi ya kurudi duniani mara nyingine tupate kufanya matendo ya kumfanya Allah Mtukufu Awe radhi na sisi? Hakika wamepata hasara nafsi zao kwa kuingia Motoni na kukaa milele humo, na vimewaondokea vile ambavyo walikuwa wakiviabudu badala ya Allah Mtukufu na yale ambayo walikuwa wakiyazua miongoni mwa yale ambayo Shetani alikuwa akiwaahidi nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net