Al-A'raaf 7:51
الأعرافٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا ۚ فَٱلْيَوْمَ نَنسَىٰهُمْ كَمَا نَسُوا۟ لِقَآءَ يَوْمِهِمْ هَـٰذَا وَمَا كَانُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَجْحَدُونَ
Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo sisi tunawasahau kama walivyousahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kama walivyo usahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu. [51]
[51] Hawa makafiri ndio ambao hawakufanya juhudi kutafuta Dini ya Haki, lakini ikawa dini yao ni kufuata pumbao na matamanio, ndio pumbao la kujipumbazia na upuuzi wa kuchezea, na maisha ya dunia na anasa zake zikawakhadaa, wakadhania hayo tu ndiyo maisha, na wakasahau kukutana nasi! Basi Siku ya Kiyama Sisi tutawasahau. Na wao hawato istarehea Pepo, na watauonja Moto, kwa sababu ya sahau yao kuisahau Siku ya Kiyama, na kuzikanusha Ishara zenye kubainika wazi, zinazo thibitisha Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale ambao Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Atawanyima starehe za Akhera ni wale ambao waliifanya Dini, ambayo Allah Mtukufu Amewaamuru kuifuata, kuwa ni pumbao, na yakawadanganya wao maisha ya ulimwenguni, wakashughulishwa na mapambo yake wasifanye matendo ya kuwafaa Akhera, hao Atawasahau Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, na Atawaacha ndani ya adhabu iumizayo, kama walivyoyaacha matendo ya kuwafaa kwa kukutana na Siku yao hii, na kwa kuwa wao walikuwa wakizikanusha dalili za Allah Mtukufu na hoja Zake pamoja na kujua kwao kuwa ni za ukweli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net