Al-A'raaf 7:45
الأعرافٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ كَـٰفِرُونَ
Wale wanaozuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka ipotoke, nao wanaikufuru Akhera.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale ambao walikuwa wakizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wakataka kuipotosha, nao wanaikanusha Akhera. [45]
[45] Hawa madhaalimu ndio wanao wazuia watu wasende kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu wa Haki, nayo ndiyo Imani na kutenda mema; na wanaweka vikwazo, na shakashaka, ili hiyo Njia yende upogo iwapoteze watu wasiweze kuifuata. Na hao wanaikanusha Akhera hawaiogopi adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makafiri hawa ndio wale waliokuwa wakiipuuza njia ya Allah Mtukufu iliyolingana sawa, na wakiwazuia watu wasiifuate, na wakitaka kwamba njia ya kuifuata iwe kombo ili kusiwe na yoyote wa kuielewa; na wao, kuhusu Akhera na mambo yake, ni wenye kukanusha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net