Al-A'raaf 7:46
الأعرافوَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى ٱلْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّۢا بِسِيمَىٰهُمْ ۚ وَنَادَوْا۟ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ أَن سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ
Na baina yao (makundi mawili hayo) patakuwapo pazia. Na juu ya Minyanyuko patakuwa watu watakaomjua kila mmoja kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Salamu Alaykum (amani iwe juu yenu)! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na baina ya makundi mawili hayo patakuwapo pazia. Na juu ya Mnyanyuko patakuwa watu watakao wajua wote kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Assalamu Alaykum, Amani juu yenu! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai. [46]
[46] Na baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni patakuwa na pazia kuzuia kufikia kwenye Mnyanyuko - na hapo ni pahala palipo nyanyuka palipo juu. Watu katika bora ya Waumini na watukufu wao, watakuwa wanawaangalia khalaiki wote hao, na wanawajua wema na waovu kwa alama zinazo onyesha ut'iifu wao na uasi wao. Wataitwa watu wema kabla ya kuingia Peponi, na hali wao wanataraji kuingia humo, watawabashiria kwa Imani na utulivu na kuingia Peponi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na baina ya watu wa Peponi na watu Motoni patakuwa na kizuizi kikubwa kinaitwa Al-A‛rãf. Na juu ya kizuizi hiki kutakuwa na wanaume wanaowajua watu wa Peponi na watu wa Motoni kwa alama zao kama weupe wa nyuso za watu wa Peponi na weusi wa nyuso za watu wa Motoni. Wanaume hawa ni watu ambao vitendo vyao vizuri na viovu viko sawasawa, na wao wana matumaini ya kupata rehema za Allah Mtukufu, (Aliyetukuka.) Wanaume hao wa hapo Al-A‛rãf watawaita watu wa Peponi kwa maamkuzi wakiwaambia, «Salãmun ‛alaykum»(Amani iwe juu yenu.) Watu hawa wa Al-A‛rãf bado hawajaingia Peponi, na wao wana matumaini ya kuingia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net