Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 43

Al-A'raaf 7:43

الأعراف

وَنَزَعْنَا مَا فِى صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمُ ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ وَقَالُوا۟ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى هَدَىٰنَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِىَ لَوْلَآ أَنْ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ ۖ لَقَدْ جَآءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلْحَقِّ ۖ وَنُودُوٓا۟ أَن تِلْكُمُ ٱلْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Na tutaondoa kilicho katika vifua vyao cha chuki, na chini yao itapita mito. Na watasema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu), ambaye alituongoa kuyafikia haya. Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoa. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walikuja na haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Bustani mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na watasema: Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuhidi kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutuhidi. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta Haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Pepo mliyo rithishwa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyafanya. [43]

[43] Na tutazitoa chuki zote ziliomo katika nyoyo zao. Basi watakuwa katika Janna, Pepo, ndugu wenye kupendana, ikipita mito ya maji matamu mbele yao. Watasema kufurahia neema watayo ipata: Alhamdulillahi, yaani Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuonyesha Njia ya kufikia neema hizi, na akatuwezesha kuifuata. Na ingeli kuwa hakutuhidi, kutuongoa, Mwenyezi Mungu kwa kutupelekea Mitume na akatupa tawfiq, tusingeweza sisi wenyewe kufikia uwongofu. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi wametujia na wahyi wa Haki! Hapo tena Mwenyezi Mungu atawaambia: Hakika hii Pepo ni zawadi mmepewa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mmepewa kwa fadhila yangu bila ya kuwa nyinyi kutoa kitu, kama urithi. Na takrima hii mlio pata ni sababu ya vitendo vyenu vyema duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ataziondoa chuki na mafundo ndani ya vifua vya watu wa Peponi. Na miongoni mwa kukamilika neema zao ni kwamba mito ya maji itakuwa ikipita chini yao. Na watasema watu wa Peponi pindi watakapoingia humo, Shukrani ni za Allah Mtukufu Aliyetuafikia kufanya vitendo vyema ambavyo vimetupatia starehe hizi ambazo tuko nazo. Na hatukuwa tuna uwezo wa kuifuata njia iliyolingana sawa kama si Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kutuongoza kufuata njia hii na kutuwezesha kukita juu yake. Mitume wa Mola wetu wametuletea habari za ukweli za ahadi njema kwa wenye kumtii na za kuwaonya wenye kumuasi. Na wataitwa kwa kupongezwa na kukirimiwa waambiwe, «Hiyo ndiyo pepo Allah Mtukufu Aliyowapa ni urithi kwa rehema Zake na kwa mliyoyatanguliza ya Imani na matendo mema».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net