Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 42

Al-A'raaf 7:42

الأعراف

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Na wale walioamini na wakatenda mema, hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Hao ndio watu wa Bustanini. Wao watadumu humo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao amini na wakatenda mema - hatumkalifishi mtu yoyote ila kwa kiasi cha uwezo wake - hao ndio watu wa Peponi. Wao watadumu humo. [42]

[42] Na wenye kuamini na wakatenda vitendo vyema ambavyo hatumlazimishi ila kwa kiasi anavyo weza mtu, hao ndio watu wa Peponi. Watastarehe humo daima dawamu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na wakafanya vitendo vyema kwa kiasi cha uwezo wao, kwani Allah Mtukufu Hamlazimishi mtu matendo isipokuwa yale ayawezayo, hao ni watu wa Peponi, wao humo ni wenye kukaa milele, hawatoki humo kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net