Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 41

Al-A'raaf 7:41

الأعراف

لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Wana kitanda chao katika Jahannamu, na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu. [41]

[41] Huko katika Jahannamu kitanda chao ni moto, na shuka ya kujifunika ni moto. Na kwa mfano huu tutawaadhibu wanao zidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Makafiri hawa ni wenye kukalishwa milele Motoni. Watapata humo kwenye Moto wa Jahanamu tandiko chini yao, na juu yao kutakuwa na mifiniko inayowafunika. Na mfano wa mateso haya mabaya Atawatesa nayo Allah Mtukufu wale madhalimu ambao wamekiuka mipaka Yake, wakamkanusha na wakamuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net