Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 40

Al-A'raaf 7:40

الأعراف

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَٱسْتَكْبَرُوا۟ عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَٰبُ ٱلسَّمَآءِ وَلَا يَدْخُلُونَ ٱلْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ ٱلْجَمَلُ فِى سَمِّ ٱلْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Hakika wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Bustanini mle mpaka aingie ngamia katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale wanao zikanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya sindano. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wakosefu. [40]

[40] Hakika wale walio kanusha Ishara zetu zilizo teremshwa katika Vitabu, na ziliopo katika ulimwengu, na wakapanda kiburi kukataa kuhidika kwa Ishara hizo, na wala wasitubu, nawakate tamaa kupokelewa a'mali zao na kupata rehema ya Mwenyezi Mungu, na kuingia Peponi, kama alivyo kata tamaa ngamia kupita katika tundu ya sindano. Na kwa mfano huu ndio tutawaadhibu hao wenye kiburi katika kila umma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale makafiri ambao hawakuzikubali hoja zetu na aya zetu zinazojulisha upweke wetu na ambao hawakuzitumia sheria zetu kwa kiburi na majivuno, vitendo vyao maishani, na pia roho zao wakati wa kufa, havitafunguliwa milango ya mbingu. Na haiwezekani kwa makafiri hawa kuingia Peponi isipokuwa iwapo ngamia ataingia kwenye tundu ya sindano; na hilo ni muhali. Na mfano wa malipo haya tutawalipa wale ambao uovu wao umezidi na kukiuka kwao mipaka kumepindukia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net