Al-A'raaf 7:3
الأعرافٱتَّبِعُوا۟ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
Yafuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala msifuate marafiki wasaidizi wowote badala yake. Ni machache mnayoyakumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka. [3]
[3] (Enyi Watu!) Fuateni aliyo kufunulieni Mola wenu Mlezi, wala msiwafuate marafiki au walinzi wengineo badala yake Yeye, mkawa mnawaitikia wao na mkiwaomba msaada! Itakuwa kama hamkuwaidhika ikiwa mtaiacha Dini ya Mwenyezi Mungu na muifuate nyengineyo, hali ya kuwa yapo mengi ya kuzingatia katika haya mliyo funuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yafuateni, enyi watu, hayo yaliyoteremshwa kutoka kwa Mola wenu miongoni mwa Qur’ani na Sunnah (mafundisho ya Mtume) kwa kufuata maamrisho na kuepuka makatazo Na wala msiwafuate wategemewa badala ya Allah Mtukufu, kama mashetani na wasomi wa Kiyahudi na watawa wa Kinaswara. Hakika nyinyi ni mara chache mnapowaidhika na kuzingatia na mkarudi kwenye haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net