Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 4

Al-A'raaf 7:4

الأعراف

وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَا فَجَآءَهَا بَأْسُنَا بَيَـٰتًا أَوْ هُمْ قَآئِلُونَ

Maana

Na ni miji mingapi tuliyoiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipokuwa wamelala adhuhuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miji mingapi tuliiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipo kuwa wamelala adhuhuri. [4]

[4] Kwani Sisi tumekwisha iteketeza miji kadhaa wa kadhaa, kwa sababu watu wao walikuwa wakiwaabudu wasio kuwa Mwenyezi Mungu, na kwa kuwa katika mwendo wao hawakufuata Njia yake. Ikawajia adhabu yetu wakati wao wameghafilika na wametuwa usiku nao wamelala, kama yalivyo wapata kaumu ya Lut'; au wakatekezwa mchana nao wamepumzika wakati wa kujinyoosha, kama yalivyo wapata kaumu ya Shua'ib.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miji mingi tuliwaangamiza watu wake kwa sababu ya kwenda kinyume kwao na Mitume wetu na kuwakanusha. Hilo likawaletea utwevu wa duniani uliounganishwa na unyonge wa Akhera. Basi adhabu yetu iliwajia, wakati mwingine wakiwa wamelala usiku, na wakati mwingine wakiwa wamelala mchana. Allah Mtukufu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuwa ni nyakati za utulivu na mapumziko. Hivyo basi, kuja kwa adhabu kwenye nyakati mbili hizi kunababaisha zaidi na adhabu yenyewe huwa ni kali zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net