Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 2

Al-A'raaf 7:2

الأعراف

كِتَـٰبٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِى صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake, ili uonye kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini. [2]

[2] (Ewe Nabii!) Umeteremshiwa wewe Qur'ani ili uwaonye hao wanao kanya wapate kuamini, na uwakumbushe Waumini wapate kuzidi Imani yao. Basi usiingie dhiki katika kifua chako unapo ifikilisha kwa kukhofu kuwa utakanushwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hii Qur’ani ni Kitabu kitukufu, Allah Mtukufu Amekiteremsha kwako, ewe Mtume. Basi pasiwe na shaka katika kifua chako kwamba imeteremshwa kutoka kwa Allah Mtukufu. Na usiwe na wasiwasi katika kuifikisha kwa watu na kuwaonya nayo. Tumeiteremsha kwako ili uwaonye nayo makafiri na uwakumbushe Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net