Al-A'raaf 7:1
الأعرافالٓمٓصٓ
Alif Laam Miim Swaad.[1]
[1] Herufi hizi "Alif Laam Miim Swaad" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
ALIF LAM MYM 'SAAD . [1]
[1] Alif Lam Mym 'Saad. (A.L.M.S'.) Hizi ni harufi za kutamkwa ambazo zinaanzia baadhi ya Sura za Makka, kwa ajili ya kuwazindua Washirikina kuwa hakika hii Qur'ani Tukufu imeundwa kwa harufi zile zile wanazo zitamka wao. Na juu ya hivyo wao wanaemewa hawawezi kuleta mfano wake. Kadhaalika harufi hizi zinapo somwa huwazindua wao wasikilize, kwa kuwa walikuwa wananasihiwa na wakubwa zao kuwa wasiisikilize Qur'ani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Alif, Lãm, Mîm, Ṣãd.» Yametangulia maneno kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al- Baqarah.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net