Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 165

Al-An'aam 6:165

الأنعام

وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَكُمْ خَلَـٰٓئِفَ ٱلْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَـٰتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِى مَآ ءَاتَىٰكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلْعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌۢ

Maana

Naye ndiye aliyewafanya kuwa wafuatizi (makhalifa) katika ardhi, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali ili akujaribuni katika hayo aliyowapa. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [165]

[165] Na Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyeni makhalifa (walio chukua pahala pa) kaumu zilizo tangulia katika kuamirisha ulimwengu. Naye amewanyanyua baadhi yenu kuliko wengine kwa daraja nyingi katika mambo yanayo onekana na yasiyo onekana kwa vile kukupeni njia za kuyafikilia, ili apate kukujaribuni, kukufanyieni mtihani, katika hizo neema alizo kupeni, vipi mtazishukuru, na katika sharia alizo kupeni mtazitumia vipi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwepesi wa kuwaadhibu wakhalifu, kwani hakika adhabu yake itakuja tu bila ya shaka, na kila lijalo lipo karibu. Na Yeye ni mwenye maghfira makubwa kwa makosa ya wenye kutubu na wakatengenea, na Mkunjufu wa rehema kwao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyewafanya nyinyi mshike nafasi za waliowatangulia katika ardhi baada ya Allah Mtukufu kuwaondoa na kuwaweka nyinyi badala yao, mpate kuiamirisha baada yao kwa kumtii Mola wenu. Na amewainua daraja baadhi yenu, katika mapato na nguvu, juu ya wengine ili kuwapa mtihani katika alichowapa miongoni mwa neema Zake, apate kuwa wazi kwa watu mwenye kushukuru na asiyeshukuru. Hakika Mola wako ni Mwepesi wa adhabu kwa aliyemkanusha na kumuasi. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa aliyemuamini na akafanya matendo mema na akatubia na dhambi yenye kuangamiza, ni Mwenye huruma Kwake. Al-Ghafûr (Mwingi wa kusamehe)na Al-Raḥîm (Mwenye kurehemu) ni majina mawili matukufu katika majina ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net