Al-An'aam 6:164
الأنعامقُلْ أَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْغِى رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَىْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ
Sema: Je nimtafute mola mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na wala haichumi kila nafsi isipokuwa ni juu yake. Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine. Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu, kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitilafiana ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana. [164]
[164] Sema ewe Muhammad, kuwakatalia washirikina wito wao kwako, uwakubalie ushirikina wao: Nimtafute wa kumuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Muumba wa kila kitu? Na waambie kuwakatalia kuwa wao hawawezi kukubebea makosa yako ikiwa utawakubalia: Hapana nafsi inayo tenda kitu ila itapata malipo yake wenyewe peke yake. Hachukui mtu dhambi za mwenziwe. Kisha mtafufuliwa kwa Mola Mlezi wenu baada ya mauti, naye atakupeni khabari ya hayo mliyo khitalifiana kwayo duniani, katika mambo ya itikadi, na atakulipeni kwayo. Basi vipi nimuasi Mwenyezi Mungu kwa kutegemea ahadi yenu ya uwongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Kwani natafuta mola mwingine asiyekuwa Allah Mtukufu? na hali Yeye ni Muumba wa kila kitu, ni Mwenye kukimiliki na kukiendesha?» Na hafanyi Mwanadamu yoyote tendo baya isipokuwa dhambi zake zitamshukia mwenyewe, wala haitabeba, nafsi yenye dhambi, dhambi za nafsi nyingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Siku ya Kiyama, awape habari ya yale mliokuwa mkitafautiana juu yake katika mambo ya dini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net