Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 163

Al-An'aam 6:163

الأنعام

لَا شَرِيكَ لَهُۥ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلْمُسْلِمِينَ

Maana

Hana mshirika yeyote. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. [163]

[163] Hana mshirika katika kuumba, wala katika kustahiki kuabudiwa. Naye Yeye Mola Mlezi wangu ameniamrisha kwa hayo nimfanyie ikhlasi (usafi wa niya) katika Tawhidi (kutakasisha upweke wake) na vitendo. Na mimi ni wa kwanza wa kumnyenyekea, kumfuata, na mkamilifu wao wa ut'iifu na kusilimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Asiye na mshirika katika uungu Wake wala katika umola Wake wala katika majina Yake na sifa Zake. Kumpwekesha huko Allah Mtukufu kulikosafishika ndiko Alikoniamrisha mimi Mola wangu, Aliyetukuka na kuwa juu. Na mimi ni wa kwanza kumfuata Allah Mtukufu kikamilifu katika umma huu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net