Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 162

Al-An'aam 6:162

الأنعام

قُلْ إِنَّ صَلَاتِى وَنُسُكِى وَمَحْيَاىَ وَمَمَاتِى لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Sema: "Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu , na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. [162]

[162] Sema: Hakika Sala yangu na ibada zangu, na niyafanyayo katika hali ya uhai wangu, nayo ni ut'iifu, na Imani na vitendo vyema ninavyo kufa navyo, vyote hivyo nimevisafia kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu Aliye umba vitu vyote, na kwa hivyo akastahiki kuabudiwa Yeye peke yake, na kut'iiwa Yeye peke yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, Hakika Swala yangu na nusuk yangu, yaani kuchinja kwangu ni kwa ajili ya Allah Mtukufu, Peke Yake; si kwa ajili ya masanamu wala wafu wala majini wala wasiokuwa hao kati ya wale, wasiokuwa Allah Mtukufu, mnaowachinjia na kutaja majina yasiyokua jina Lake, kama mnavyofanya. Pia uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah Mtukufu, Mola wa viumbe wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net