Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 161

Al-An'aam 6:161

الأنعام

قُلْ إِنَّنِى هَدَىٰنِى رَبِّىٓ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Maana

Sema: "Hakika mimi, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye njia iliyonyooka, dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahim aliyekuwa mnyofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. [161]

[161] Sema ewe Nabii kwa kubainisha Dini ya Haki unayo ifuata: Hakika Mola wangu ameniongoza, na ameniwafikisha kuishika Njia Iliyo Nyooka, yenye kufika ukomo wa kukamilika na kunyooka. Na Dini hii ndiyo aliyo ifuata Ibrahim akaacha itikadi zote potovu. Na Ibrahim hakuwa akimuabudu mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, kama wanavyo dai washirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi Ameniongoza Mola wangu kwenye njia iliyolingana sawa yenye kufikisha kwenye Pepo Yake, nayo ni Dini ya Uislamu yenye kusimamia mambo ya dunia na ya Akhera; nayo ni Dini ya kumpwekesha Allah Mtukufu, Dini ya Ibrãhîm, amani imshukiye. Na Ibrãhîm, amani imshukiye, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha pamoja na Allah Mtukufu asiyekuwa Yeye».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net