Al-An'aam 6:160
الأنعاممَن جَآءَ بِٱلْحَسَنَةِ فَلَهُۥ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَآءَ بِٱلسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰٓ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Mwenye kuja na jema, basi ana mara kumi mfano wake. Na mwenye kuja na baya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake. Na wao hawatadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa. [160]
[160] Mwenye kutenda mema atalipwa thawabu zake mpaka mara kumi kwa kufadhiliwa na kukirimiwa. Na mwenye kutenda ovu hatoadhibiwa ila kwa kadri ya maasi yake tu, kwa uadilifu wake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hapo hapana dhulma kwa kumpunguzia mtu thawabu, wala kumzidishia adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kukutana na Mola wake, Siku ya Kiyama, akiwa na jema moja miongoni mwa matendo mazuri, atapata mema mfano wake mara kumi. Na mwenye kukutana na Mola wake akiwa ana ovu moja, hatateswa isipokuwa kadiri ya mfano wa ovu hilo, na wao hawatadhulumiwa hata kiasi cha uzito wa (mduduchungu).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net