Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 159

Al-An'aam 6:159

الأنعام

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَرَّقُوا۟ دِينَهُمْ وَكَانُوا۟ شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِى شَىْءٍ ۚ إِنَّمَآ أَمْرُهُمْ إِلَى ٱللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ

Maana

Hakika wale waliofarakisha Dini yao na wakawa makundi makundi, wewe si miongoni mwao katika chochote. Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna ukhusiano nao wowote. Bila ya shaka shauri yao iko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawaambia yale waliyo kuwa wakiyatenda. [159]

[159] Hakika walio igawanya Dini moja ya Haki kwa itikadi za uwongo, na sharia za upotovu, na wakawa kwa sababu hiyo makundi mbali mbali; unawadhania ni wamoja, kumbe nyoyo zao zimekhitalifiana, wewe huna jukumu kwa kufarikiana kwao na uasi wao, wala wewe huwezi kuwahidi. Wewe hulazimiki ila kufikisha Ujumbe. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki mambo yao kwa kuwaongoa na kuwalipa, kisha awatajie Siku ya Kiyama yale waliyo kuwa wakiyafanya duniani na awalipe kwayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walioigawanya dini yao, baada ya kuwa mkusanyiko mmoja juu ya kumpwekesha Allah Mtukufu na kufuata sheria Yake kivitendo, wakawa ni makundi na mapote, wewe, ewe Mtume, uko mbali na wao. Hukumu yao iko kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kisha Yeye Atawapa habari za matendo yao, Amlipe aliyetubia miongoni mwao na akafanya wema, kwa wema wake na Amtese mtenda maovu kwa uovu wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net