Al-An'aam 6:158
الأنعامهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِىَ بَعْضُ ءَايَـٰتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِى بَعْضُ ءَايَـٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَـٰنُهَا لَمْ تَكُنْ ءَامَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِىٓ إِيمَـٰنِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓا۟ إِنَّا مُنتَظِرُونَ
Je, wanangoja isipokuwa kwamba wajiwe na Malaika, au awajie Mola wako Mlezi, au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake. Sema, "Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja. [158]
[158] Hoja imekwisha simama ya kuwa kuamini ni waajibu. Na watu hawa hawakuamini. Basi wanangojea nini ndio waamini? Je, wanangojea wawajie Malaika wawe ni Mitume badala ya kuwa wanaadamu, au wawe ni mashahidi kushuhudia ukweli wako? Au aje Mwenyewe Mola wako Mlezi, wamwone, au ashuhudie ukweli wako? Au zije baadhi ya alama za Mola wako Mlezi zishuhudie ukweli wako? Na pindi zikija hizo alama za Mola wako Mlezi za kuwapelekea kuamini, basi Imani yao haitowafaa kitu. Kwani hiyo itakuwa ni Imani ya kahari, hawana hila. Na sasa tena haimfalii mwenye kuasi toba yake na ut'iifu wake. Kiwango cha kufanya waajibu kimekwisha pita! Waambie hawa wanao kataa na kukanusha: Ngojeni moja ya mambo hayo matatu, nanyi endeleeni katika kukanusha kwenu. Nasi pia tunangoja hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawangojei, hawa wenye kukataa na wakazuia watu wasiifuate njia ya Allah Mtukufu, isipokuwa awajie wao Malaika wa mauti na wasaidizi wake kuzichukua roho zao au aje Mola wako, ewe Mtume, kutoa uamuzi kati ya waja wake Siku ya Kiyama, au zije baadhi ya alama za Kiyama na vitambulisho vyake vinavyoashiria kuja kwake, navyo ni kuchomoza jua kutoka upande wake wa Magharibi? Basi litakapokuwa hilo hakuna nafsi yoyote itakayofaidika na Imani yake, iwapo haikuwa imeamini kabla ya hapo, wala hayatakubaliwa matendo mema mapya ya hiyo nafsi, ikiwa ilikuwa imeamini, iwapo haikuwa imeyatenda kabla ya hapo. Waambie, ewe Mtume, «Ngojeeni kuja kwake, ili mpate kumjua aliye kwenye usawa na aliye kwenye makosa, na mtenda maovu na mtenda mema. Sisi tunalingojea hilo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net