Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 28

Al-A'raaf 7:28

الأعراف

وَإِذَا فَعَلُوا۟ فَـٰحِشَةً قَالُوا۟ وَجَدْنَا عَلَيْهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأْمُرُ بِٱلْفَحْشَآءِ ۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Na wanapofanya uchafu, husema: Tuliwakuta baba zetu juu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uchafu. Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua? [28]

[28] Na wakanushao wakitenda jambo ovu la mwisho, kama shirki, na kut'ufu kwenye Al Ka'aba nao wako uchi, na mengineyo, basi wao hutoa udhuru kwa kusema: Sisi tumewakuta baba zetu wakenda mwendo huu huu, na sisi tunawafuata wao; na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hivi na ameturidhia kwa kuwa ametukiria! Waambie ewe Nabii kuwapinga kwa uzushi wao: Hakika Mwenyezi Mungu hakuamrisha mambo haya maovu! Je, mnamnasibishia Mwenyezi Mungu mambo msiyo kuwa nayo tegemeo lolote mnalo jua lina dalili ya ukweli wa kumnasibisha nalo Subhanahu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wanapofanya tendo ovu, wanajitetea kwa kusema kwamba hilo ni miongoni mwa yale waliyoyapokea kutoka kwa baba zao na kwamba hilo ni katika yale Aliyoyaamrisha Allah Mtukufu. Waambie, ewe Mtume, «Allah Mtukufu Hawaamrishi waja Wake vitendo vichafu na viovu. Je, mnasema, kumsingizia Allah Mtukufu msiyoyajua, urongo na uzushi?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net