Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 27

Al-A'raaf 7:27

الأعراف

يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ كَمَآ أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ ٱلْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْءَٰتِهِمَآ ۗ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا جَعَلْنَا ٱلشَّيَـٰطِينَ أَوْلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Enyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani ile, akawavua vazi lao ili awaonyeshe tupu zao. Hakika yeye anawaona yeye na kabila yake kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Eny wanaadamu! Asije Shet'ani kukufitinini kama alivyo watoa wazazi wenu Peponi, akawavua nguo zao kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye na kabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashet'ani kuwa ni marafiki wa wasio amini. [27]

[27] Enyi wanaadamu! Msimuitikie Shetani na upotovu wake, mkatoka kwenye neema hizi, ambazo hazidumu ila kwa kushukuru na kut'ii, kama walivyo muitikia wazazi wenu, Adam na mkewe, akawatoa Shetani kwenye neema na ukarimu, na akawavua nguo zao zikaonekana tupu zao. Basi yeye Shetani na wasaidizi wake wanakujieni kwa namna msio watambua, wala hamuhisi mipango yao na vitimbi vyao! Lakini Shetani hana madaraka juu ya Waumini. Sisi tumemfanya yeye na wasaidizi wake kuwa ni marafiki wa wale wasio amini Imani ya kweli yenye kulazimikana na ut'iifu ulio timia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi wanadamu! Asiwadanganye Shetani akawapambia maasia, kama alivyowapambia wazazi wenu, Ãdam na Ḥawwã’, akawatoa Peponi kwa sababu hiyo, akawavua vazi lao ambalo Allah Mtukufu Aliwasitiri nalo ili tupu zao zifunuke. Shetani na kizazi chake na viumbe wa jinsi yake wanawaona nyinyi, na nyinyi hamuwaoni, basi jichungeni nao. Hakika sisi tumewafanya Mashetani ni wategemewa wa makafiri ambao hawampwekeshi Allah Mtukufu wala hawawaamini Mitume Wake wala hawautumii muongozo Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net