Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 26

Al-A'raaf 7:26

الأعراف

يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَٰرِى سَوْءَٰتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ

Maana

Enyi wanadamu! Hakika tumewateremshia vazi la kuficha tupu zenu na vazi la pambo. Na vazi la ucha Mungu, hilo ndilo bora zaidi. Hilo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka. [26]

[26] Enyi Binaadamu! Sisi tumekuneemesheni. Tumekuumbieni nguo kusitiri tupu zenu, na vitu vya pambo. Lakini ut'iifu ndio nguo bora ya kukukingeni na adhabu. Neema hizo ni katika Ishara zenye kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu, na rehema yake, ili watu waukumbuke utukufu wake. Yeye tu ndiye anaye stahiki Ungu. Na kisa hichi ni katika nyendo za Mwenyezi Mungu za uumbaji wake, zinazo bainisha nini malipo ya kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu, ili watu wakumbuke, na wafanye pupa kumt'ii Allah na kumshukuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi wanadamu, tumewaekea vazi lenyi kusitiri tupu zenu, nalo ni vazi la lazima, na vazi la pambo na kujirembesha, nalo ni vazi la kujikamilisha na kujifurahisha. Na vazi la uchaji Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo, ndilo vazi bora kwa aliyeamini. Hayo Ndiyo ambayo Allah Mtukufu Amewaneemesha nayo miongoni mwa alama za umola wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, upweke Wake, wema Wake na rehema Zake kwa waja Wake, ili mpate kuzikumbuka neema hizi na mumshukuru Allah Mtukufu juu yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net