Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 199

Al-A'raaf 7:199

الأعراف

خُذِ ٱلْعَفْوَ وَأْمُرْ بِٱلْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْجَـٰهِلِينَ

Maana

Chukua yaliyo mepesi (katika matendo yao), na amrisha mema, na jitenge na majahili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili. [199]

[199] Ewe Nabii! Waachilie mbali hao majaahili, na endelea katika njia ya Da'wa (Wito). Na wachukulie watu kwa lilio wepesi kwao. Na waamrishe kila jambo linalo pendeza na kuingia akilini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kubali, ewe Nabii, wewe na wafuasi wako kiwango cha kati cha tabia za watu na vitendo vyao, wala usitake kutoka kwao mambo magumu ili wasije wakachukia; na amrisha kwa kila neno jema na kitendo kizuri; na jiepushe na kushindana na mafidhuli na usijisawazishe na wajinga wenye uchache wa akili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net