Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 200

Al-A'raaf 7:200

الأعراف

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ نَزْغٌ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ ۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na kama uchochezi kutoka kwa Shetani utakuchochea, basi tafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi mzuri, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na uchochezi wa Shet'ani ukikuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi, Mjuzi. [200]

[200] Na Shetani akikuchochea kwa wasiwasi ili apate kukuachisha ulio amrishwa, kama vile kukasirika kwa kukushikilia kwao mambo ya shari, basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu akuepushe naye huyo Shetani. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na kujua kila linalo tokea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo utashikwa na hasira, ewe Nabii, zitokazo kwa Shetani au ukahisi, kutoka kwake, wasiwasi au ulegevu wa kufanya mema au himizo la kufanya ovu, basi tafuta himaya kwa Mola wako kwa kujilinda Kwake. Kwani Yeye ni Msikizi wa kila neno ni Mjuzi wa kila kitendo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net