Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 198

Al-A'raaf 7:198

الأعراف

وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى ٱلْهُدَىٰ لَا يَسْمَعُوا۟ ۖ وَتَرَىٰهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ

Maana

Na mkiwaita kwenye uongofu, hawasikii. Na utawaona wanakutazama hali ya kuwa hawaoni.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkiwaita kwenye uwongofu hawasikii. Na unawaona wanakutazama, nao hawaoni. [198]

[198] Na ukiwataka uwongofu katika yaliyo na kheri nanyi hawalisikii ombi lenu, licha ya kukuongozeni! Unawaona wanavyo kukabili kama kwamba wanakutazama, na kumbe wao kwa hakika hawaoni kitu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo mtawaita, enyi washirikina, hao waungu wenu kwenye kulingana sawa na haki hawatasikia mwito wenu. Na utawaona, ewe Mtume, waungu wa hawa washirikina miongoni mwa wenye kuabudu mizimu, wanakuelekea kama wanaokutazama na hali wao hawaoni kwa kuwa wao hawana macho wala busara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net