Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 196

Al-A'raaf 7:196

الأعراف

إِنَّ وَلِـِّۧىَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى نَزَّلَ ٱلْكِتَـٰبَ ۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّـٰلِحِينَ

Maana

Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu ambaye aliteremsha Kitabu. Naye ndiye anayewalinda walio wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu aliye teremsha Kitabu. Naye ndiye awalindae walio wema. [196]

[196] Hakika msaidizi wangu wa kuninusuru nanyi ni Yeye Mwenyezi Mungu. Ulinzi wangu uko kwake. Naye ndiye aliye niteremshia Qur'ani. Na Yeye peke yake ndiye anaye wanusuru waja wake walio wema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika mtegemewa wangu ni Allah Mtukufu Ambaye Anasimamia kunihifadhi na kunipa ushindi. Yeye Ndiye Ambaye Aliniteremshia Qur’ani kwa haki na Yeye Anawasimamia walio wema miongoni mwa waja wake na anawapa ushindi juu ya maadui zao na Haachi kuwasaidia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net