Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 195

Al-A'raaf 7:195

الأعراف

أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَآ ۖ أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَآ ۖ أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَآ ۖ أَمْ لَهُمْ ءَاذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۗ قُلِ ٱدْعُوا۟ شُرَكَآءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ

Maana

Je, wao wanayo miguu wanayotembea kwayo? Au wanayo mikono wanayokamata kwa nguvu kwayo? Au wanayo macho wanayoona kwayo? Au wanayo masikio wanayosikia kwayo? Sema: Waiteni washirika wenu hao, kisha nifanyieni mimi njama, na wala msinipe muhula.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, wao wanayo miguu ya kwendea? Au wanayo mikono ya kutetea? Au wanayo macho ya kuonea? Au wanayo masikio ya kusikizia? Sema: Iiteni hio miungu yenu ya ushirikina. Kisha nifanyieni mimi vitimbi, wala msinipe muhula. [195]

[195] Bali haya masanamu ni duni kuliko nyinyi kwa kuumbwa na kuwa! Kwani wao wana miguu ya kuendea? Au wana mikono ya kukinga madhara yasikupateni au yasiwapate wenyewe? Au wana macho ya kuonea? Au masikio ya kusikia hayo mnayo yataka wakakupeni? Hawana chochote katika hayo! Vipi basi mnawashirikisha hao na Mwenyezi Mungu? Na ikiwa nyinyi mnadhani kuwa hio miungu ya uwongo inaweza kunidhuru mimi au mtu yeyote, basi iiteni, na mfanye njama zenu pamoja nao kama mtakavyo, bila ya kunipa muhula wala kungoja. Hao hakika hawawezi kitu! Basi msiningojee, na wala mimi siwabali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, waungu hawa na masanamu wana miguu ya kutembelea na nyinyi katika haja zenu? Au wao wana mikono ya kuwatetea na kuwanusuru juu ya anayewatakia shari na maovu? Au wao wana macho ya kutazamia, wakapata kuwajulisha yale waliyoyashuhudia na wakayaona miongoni mwa yale yaliyofichika kwenu mkawa hamuyaoni? Au wao wana masikio ya kusikia kwayo, wapate kuwapa habari ya yale msiyoyasikia? Iwapo waungu wenu ambao mnawaabudu hawana vitu hivi, kuna maana gani kuwaabudu, ilhali wao hawana vitu hivi ambavyo kwavyo kunapelekea kujipatia manufaa au kujiepushia madhara? Waambie, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wenye kuwaabudu masanamu, Waiteni waungu wenu ambao mliwafanya ni washirika wa Allah Mtukufu katika ibada, kisha kusanyikeni kunifanyia ubaya na maudhi, msinipe muhula na lifanyieni haraka hilo, kwani mimi siwajali waungu wenu kwa kuwa nategemea hifadhi ya Allah Mtukufu Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net